Zifuatazo ni sifa za kujiunga BURUTE SACCOS LTD
1.Awe mwenye umri usiopungua miaka 18
2.Awe na tabia nzuri na akili timamu
3.Awe amelipa kiingilio na hisa, na awe anaweka akiba.
4. Awe mwaminifu na mwadilifu
5.Awe tayari kufuata masharti ya chama.
6.Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa au kuandikishwa na anayekubalika kwenye masharti ya BURUTE SACCO.
7.Awe wa kuaminika na kufahamika na wanachama wenzake.
8.Awe Mfanyakazi wa umma aliyeajiriwa/aliyestaafu kazi akiwa mwanachama
9.Awe tayari kushiriki kikamilifu katika shughuli zote za Chama
10.Asiwe na shughuli binafsi zinazofanana na shughuli za Chama
11.Awe amelipa kiingilio na kununua kima cha chini cha Hisa.
12.Awe tayari kufuata sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 20 ya Mwaka 2003 na Marekebisho yake pamoja na Kanuni za Ushirika za Mwaka 2004 na Masharti ya Chama
--
--