sababu za ukomo wa uanachama

❖Akiwa na Ugonjwa wa Akili uliothibitika.

❖Akipatikana na hatia ya jinai ambayo itasababisha afungwe jela.

❖Kutohudhuria Mikutano ya Chama mara tatu mfululizo bila sababu za msingi.

❖Kufukuzwa Uanachama na theluthi mbili (2/3) ya Wanachama waliohudhuria katika Mkutano Mkuu wa Chama baada ya kupewa nafasi ya kujitetea.

❖Kujiuzulu kwa Hiari yake.

❖Kwa sababu zozote zilizomo kwenye Kanuni za Ushirika za Mwaka 2004 kifungu cha 25.

❖Kushindwa kulipa Mkopo wake katika muda ulioruhusiwa na Chama pasipo kuwa na sababu yeyote inayokubalika na Bodi ya Chama.

❖Kufanya kitendo chochote ambacho Bodi itaridhika kuwa ni cha kutokuwa mwaminifu au ambacho ni kinyume na madhumuni ya Chama. Kusimamishwa kwa sababu hii lazima kuthibitishwe na Mkutano Mkuu wowote utakaoitishwa mapema.

❖Kuacha kushiriki katika shughuli za Chama kama kuweka Akiba kwa muda uliopangwa.

❖Kufungwa jela kwa muda usiopungua miezi sita kwa kosa la jinai hususani la kutokuwa mwaminifu.

❖Kuchukua Hisa zake zote kwenye Chama.

❖Ugonjwa wa akili uliothibitishwa na Daktari wa tiba anayetambulika.

❖Kujiuzulu/Kuacha Uanachama mwenyewe baada ya kutoa taarifa ya siku 90 kwa maandishi na awe hadaiwi na Chama. Hata hivyo haki zake za Gawio hazitalipwa mpaka hesabu kwa kipindi hicho yawe yamekamilika na kukubaliwa na Mkutano Mkuu.

❖Kufukuzwa uanachama katika Mkutano Mkuu kwa kura ya wanachama wasiopungua theluthi mbili (2/3) ya waliohudhuria, baada ya kupewa nafasi ya kujitetea kutokana na makosa ( kama yalivyo ainishwa kwenye Sheria ya vyama vya Ushirika namba 6 ya mwaka 2013) ambayo yanasababisha kufukuzwa huko.

❖Kifo cha Mwanachama.

Kusimamishwa/Kufukuzwa Uanachama

❖Kwa mujibu wa Masharti ya Chama, Bodi ya Chama itawasilisha kwenye Mkutano Mkuu majina ya Wanachama ambao kwa nyakati tofauti wataonekana kutenda makosa ambayo yanaenda kinyume na Kanuni na Taratibu za Chama kama ifuatavyo;

❖Kutoheshimu na kutotekeleza maamuzi ya Mikutano Mikuu na vikao vya Bodi ya Chama.

❖Kutolipa Hisa na ada mbalimbali za Chama baada ya kupewa muda uliokubaliwa na Mkutano.

❖Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama.

❖Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama, Kanuni na Sera za Chama.

❖Kubainika kutoa au kupokea rushwa katika utekelezaji wa shughuli za Chama.

❖Wizi.

❖Sababu zozote zilizomo katika kifungu cha 26 cha Kanuni za Ushirika za Mwaka 2004.

❖Mwanachama aliyejiuzulu au kufukuzwa Uanachama anaweza kujiunga tena kwa kuomba upya na taratibu za kujiunga na Chama zitazingatiwa.